Prof.Ndakidemi alia na vifaa tiba kituo cha Afya Uru kusini


 DODOMA

Mbunge wa Jimbo Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro,(CCM)Prof.Patrick Ndakidemi ameiomba Serikali kupeleka vifaa tiba vya kisasa katika kituo cha Afya Uru kusini ,ambacho kinatarajiwa kuanza kutoa huduma.








Prof. Patrick Ndakidemi akiuliza swali la nyongeza bungeni leo Juni 11,2024 ,je ?serikali inampango gani wa kununua vifaa tiba katika kituo cha Afya Uru kusini ambacho ni kipya na kinatarajiwa kuanza kutoa huduma karibuni?

Amesema  kupelekwa kwa vifaa tiba katika hicho kitawaondolea wananchi wa Uru kusini pamoja kata jirani za Jimbo la Moshi vijijini na baadhi kata za majimbo mawili ya Vunjo na Moshi mjini adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma.


Akijibu swali hilo, Waziri Ummy alisema kuwa, kupitia bajeti ya fedha ya Ofisi ya Rais na Serikali za mitaa Tamisemi na Wizara ya Afya wametenga fedha kwa ajili ya kununua vifaa tiba na vitasambazwa katika vituo vyote vya Afya. 

Alisema kuwa, na hii ni kazi nzuri ambayo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameifanya katika nchi kuhakikisha vifaa tiba vya kisasa vinapatikana katika ngazi ya zahanati na ngazi ya vituo vya Afya. 

Waziri huyo Ali kuhakikisha Mbunge Ndakidemi wananchi wa Uru kusini watapata vifaa tiba kabla ya uchaguzi mkuu mwakani..


"Waziri Ummy umenisaidia sana kwenye Jimbo langu kunipatia vifaa tiba katika vituo vya Afya Umbwe na Uru kiasini je serikali inampango gani wa kutusaidia vifaa tiba katika kituo cha Afya Uru kusini ambacho ni kipya na kinatarajiwa kutoa huduma karibuni" Alihoji Prof. Ndakidemi. 

Mwisho...




Post a Comment

0 Comments