DC MOSHI KULA SAHANI MOJA NA MASHOGA NA WASAGAJI


 


Safina Sarwatt,Moshi,










MKUU wa wilaya Moshi Godfery Mzava ametangaza vita dhidi  ya wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja(MASHOGA)pamoja na wanawake wanaojihusisha na vitedo vya  usagaji.


Ametangaza vita hivyo hivi karibuni kwenye kikao cha bazara la kikanuni la umoja wa wanawake wa chama cha Mpinduzi CCM (UWT)wilaya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.

 

“Kuna changamoto kubwa sana hapa moshi vijana wetu kuangukia katika wimbi kumbwa la unywaji wa pombe haramu gongo pamoja na  vitendo vya usagaji na  ushoga  na kushindwa kutoa mchangao wao katika shughuli za maendeleo,”

Alisema Changamoto ya vitendo vya ushonga kwenye wilaya moshi ni kubwa lakini watu wanashindwa kuvisemea kutokana na kuona aibu.


Alisema serikali ya awamu ya sita chini ya   Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan haikubaliane n'a vitendo hivyo ambavyo vinadhalilisha utu na kwamba lazima Sheria ichukue mkondo wake kwa watu wanaojihusisha na vitedo hivyo.

 

 

"Serikali yenu ya awamu ya sita chini ya jemedali wake Dkt.Samia Suluhu Hassan haitafumbia macho vitendo hivyo,hatuwezi kuwa na vijana ambao muda wote wamelewa na kufanya vitendo vya kudhalilisha utu",alisema.

Alitumia kikao hicho kuwaasa kina mama  kuwaonya vijana ambao wanaenda kinyume na  maadili na kwamba serikali haiwezi kuwa na kundi kubwa la vijana tegemezi  ambao hawawezi kufanyakazi kutokana na kujikita kwenye ulevi.

 

Aliitaka jumuiya hiyo ya wanawake ya CCM kuwa  kuwa mstari wa mbele kusaidia  malezi ya vijana kwa kuwaasa waachane na vitendo vya ushonga,usagaji na ulevi pamoja  na matumzi ya dawa za kulevya.

 

"Naomba niwaambia kwamba katika vitendi hivyo na mimi ninaomba niwe sadaka kupambana na vita hivyo vya usagaji na ushonga kwa kweli hatuwezi kufumbia macho vitendo hivyo",alionya .

 

“Najua ni jambo nzito, watu wenye fedha  wanafanya vitendo hivyo kwa siri na kuwarubuni vijana lakini kwa sababu sheria zipo ,niwaombe mama zangu  muwe sehemu ya  mapambano haya",alisema.


Aliomba   ushirikiono katika mapambano dhidi ya vitendo hivyo hata kama tatizo hilo   halitamalizwa ndani ya muda mfupi lakini lazima jamii ione  kwamba serikali haikubaliani na  jambo hilo ambalo alisema haliendani na maadili ya kiafrika.




Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro,Mecy Mollel alisema kama chama wako tayari kupambana na vietendo hivyo ya ushoga ambavyo alisema vinadhalilisha utu na kushusha heshima ya watoto wa kiume.

Alisema kuwa vijana  wengi wamejiingiza katika vitendo vya usagaji na ushonga kutokana na matumizi ya dawa za kulevya na unywa wa pombe haramu.

Alisema kuwa chama hicho  kinahitaji wapiga kura lakini pia kinahitaji nguvu kazi ya taifa yenye maadili mema na uadhlifu.

Alisema kuwa vitendo hivyo vimesababisha watu kutokuwa na uwezo wa kuzaliana hivyo baadhi ya shule kukokasa wanafunzi.

 

Naye mbunge wa jimbo la Moshi mjini Priscus Tarimo alisema kuwa serikali ya  awamu ya sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassana imeleta fedha nyingi katika manispaa ya Moshi zikiwamo za   ujenzi wa uwanja ndogo wa ndege wa Moshi na kwamba hakuna sababu ya Rais Samia kukosa kura za kutosha katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2025.


Alisema kuwa serikali imetekeleza miradi mingi ya maendeleo hakuna haja ya kujibishana na mtu wala kuchambua na kutukana na watu na kiwataka  wanaCCM  tujivunie hilo.

 

Alitaja maeneo ambayo fedha hizo zitumika ikiwa ni pamoja na jengo la Mama na Mtoto katika Hospital ya rufaa ya mkoa ya  mawenziuboreshwaji was vifaa vya afya .

Maeneo mengine ni kuboreshwa kwa upatikana wa maji safi na salama kwa  asilimia100 ,huduma  ya meme ambako wananchi wengi wameunganishwa kwenye huduma hiyo wananchi  huku serikali ikiboresha elimu kwa shule nyingi kuwa na vyumba vingi vya   madarasa yakiwamo  yaliyojengwa  katika viwango vya ubora unaotakiwa.



mwisho





Post a Comment

0 Comments