Safina Sarwatt,
MOSHIWanachama 71 wa Chama cha msingi cha ushirika(AMCOS)cha Kirima Boro wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro wamepaza sauti wakimuomba Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi kurejeshwa kwenye chama hicho Ekari 37 ambazo zimeuzwa kinyemela kwa watu wasiowanachama.
Ekari hizo 37 ambazo ni sehemu ya shamba kubwa la Antippi linalomikiwa na Chama hicho,inadaiwa ziitengwa na serikali kwa ajili ya kupanua Taasisi za kijamii zikiwamo shule za Msingi Kidachini,Masoka na Ngirinyi.
Mbali na shule hizo,ekari hizo pia zilikuwa zinufaishe upanuzi wa Kanisa katoriki Kirima,Msikiti wa Kirima,ujenzi wa ofizi ya kata ya Ngirinyi pamoja na ujenzi wa kituo cha afya.
Hata hivyo tofauti na matarajio ya wananchi,ekari hizo zinadaiwa kuuzwa kwa watu wasiohusika na ambao si walengwa na wanachama hao kutaka zirejeshwe mikononi mwao ili apewe mwekezaji VASSO AGROVENTURE LTD.
“Sisi wanachama tuliorodhesha majina hapo chini kutoka chama cha msingi Kirima Boro AMCOS LTD kwa kauli moja tumeafikia kuwa shamba la ekari 37 zilizotengwa kwa ajli ya Taasisi lirudishwe lirudishwe Antippi Estate ili tumkabidhi mwekezaji Vasso Agroventure LTD”,inasema barua hiyo.
Barua hiyo ikaungwa mkono na barua ya mtu aliyejitambulisha kama mdau wa maendeleo kata ya Kibosho Kirima ya Agosti 28 mwaka juzi kwenda mkuu wa wilaya ya Moshi .
Barua hiyo imebeba kichwa cha habari na hapa nanukuu “YAH
Mdau huyo ameandika “,Naomba kukujulisha kuwa kuna ekari 37 za sehemu ya shamba la Antippi za sehemu ya shamba la Antippi Estate ambazo zimeporwa na kumilikiwa na watu ambao siyo walengwa waliokusudiwa kuhamishiwa eneo hilo ili kuruhusu upanuzi wa Taasisi za serikali na za kijamii”,ameandika.
Kwa mujibu wa mdau huyo ambaye amewahi kushika wadhifa wa kiongozi wa kisiasa,amedai kuwa alipokuwa kiongozi wa eneo hilo moja ya kero aliyokabidhiwa na wananchi ni kushughulikia ufisadi huo.
Anasema ardhi iliyoporwa ya ekari 37 ni sehemu ya shamba la Antippi lenye Hati Miliki Namba 16827 ambayo ilimikishwa kwa chama cha msingi cha Ushirika(AMCOS) Kirima Boro kwa lengo la kuliendeleza ikiwamo kuliwekeza na kuchukua kodi ya pango kutoka kwa mwekezaji wa kilimo cha zao la kahawa.
“Katika kipindi changu cha uongozi niliamini kuwa jambo hilo ni jepesi kulipatia suluhu ya kudumu baada ya kujulishwa waliogawa aridhi hiyo kwa watu wasiohusika ni wakibosho wa vijiji vya Kiirma kati na Boro,tena ambao waliwahi kushika nafasizauongozi wa vijiji na ushirika”,anasema kwenye barua yake.
Barua hiyo ya mdau wa maendeleo Kibosho yenye kurasa 13 inahitimisha kwa kumwomba mkuu wa wilaya kuchukua hatua dhidi ya waliohusika na ufisadi wa ardhi ya wanaushirika.
0 Comments