Safina Sarwatt,Serengeti,
Kampuni ya wakala
wa Utalii nchini ya Zara Tanzania Adventures.imeanzisha
kampeni ya kila mwezi Desemba
kuhamasisha Watanzania kwenda kutembelea vivuto vya utalii katika Hifadhi ya taifa ya Serengeti itwayo
“TWENDE ZETU SERENGETI
Lengo la
kampeni hiyo ni katika jitihada za kuunga
mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kukuza utalii wa ndani na
kuongeza ajira kwa vijana.
Hii ni
kampeni ya pili katika kuhamasisha watanzania kutembelea vivutio vya utalii
baada ya ili ya awali ya “TENDE ZETU KILELLENI”ambayo ni mahususi katika
kusherehekea siku ya uhuru wa Tangaznyika ambayo hufanyika kila Desemba 5 kila
mwaka.
Ni tukio
ambalo huwakutanisha watanzania wengi katika kupanda mlima Kilimanjaro na
kufika kilele cha Uhuru Desemba 9 mbayo ndiyo siku ya Uhuru.
Kampeni ya “TWENDE
ZETU SERENGETI,”sasa imeingia msimu wake wa tatu tangu kuanzishwa kampeni
inayoonekana kuleta mwamko mkubwa kwa Watanzania kutokana na kujitokeza kwa
wingi kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti .
Mkurugenzi
wa kampuni Zara Tanzania Adventures ,Zainab Ansell mwanzilishi wa kampeni hiyo
anasema kampeni hiyo itakuwa endelevu ikiwa ni mkakati wa kuhasisha watanzaia
kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii.
Kwa upande
wake Rafael Masaki kutoka idara ya Masoko ya kampuni hiyo ya Zara anasema kampeni
hiyo inalenga kuchochea utalii wa ndani pamoja na kutangaza vivutio vya utalii
vilivopo nchini.
Mwaka jana
kampuni hiyo ilitoa ofa kwa watanzania kutembelea hifadhi za Taifa za Tarangire,Manyara,Serengeti
pamoja na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorogoro kwa gharama nafuu ya sh,850,000 ikihusisha
chakula na malazi kwa siku mbili katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti .
Raphael
aansema kuwa zara imekuwa ikitoa michango mikubwa katika kuhakikisha wanatoa
huduma bora kwa wageni wote wanatembelea Serengeti kwa gharama nafuu ya
shilingi 850,000/= mtu moja na watoto miaka (14) 450,000/= kwa siku mbili ndani
ya hifadhi ya Serengeti.
Anasema kuwa
idadi ya watalii wanaojitokeza kushiriki kampeni hiyo ya “twende zetu
Serengeti” imeongezeka ikilinganishwa na
mwaka 2023 hii ni kutokana na huduma
nzuri inayotolewa na kampuni hiyo.
Anasema
kampuni hiyo imeona umuhimu wa kutangaza
utalii kupitia kampeni hiyo ikiwa ni mikakati ya kuhakikisha wanaunga mkono
juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kutangaza utalii wa ndani ili
kuongeza mapato ya taifa na soko la uhakika la utalii.
Mbali na
kampeni hiyo ,Zara Tours wamekuja na progamu mpya ya kwende Serengeti siku ya
wapendano kila mwaka mwezi wa nne na kwa mwaka wanafanya kampeni ya kupeleka
wageni mara tatu .
Alisema
kampeni hiyo itaweza kuleta hamasa kubwa kwa watanzania pamoja na kuchochea uchumi wa nchi kupitia sekta ya utalii.
Joseph
Chitinka mmoja wa watalii wa ndani na mkazi wa Dodoma waliotembelea vivutio vya
utalii kupitia kampeni hiyo,alitoa wito kwa watanzania kuthamini rasilimali za ndani ikiwamo kuzitangaza.
“Nitoe wito
kwa watanzania wenzangu kujenga utamaduni wa
kutembelee vivutio vya utalii kwani
kwa kufanya hivyo itasaidia kuchochea uchumi wa taifa na uchumi wa mtu mmoja mmoja”.alisema.
anasema Rais
Dkt.samia Suluhu Hassan alishafungua
milanga baadaya kuzindu giamu ya Royal Tour
na kuwataka watanznaia kuunga mkono jitihada hizo za rais kwa kutembelea vivutio vya utalii na kukuza
pato la Taifa.
“Lengo la
rais kufungua kampeni yake kupitia filmu ya Royal Tour ni kukuza soko la utalii wa ndani badala
ya kutegemea watalii kutoka mataifa ya nje na hata yakitokea majanga kama ilivyotokea UVICO 19
sekta hiyo isiyumbe na makampuni ya utalii yaendelee na kazi”.
Alisema
watanzania wanapaswa kumwelewa Rais Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa na maono ya kuona
mbali kwa kuanzisha Royal tour na kwamba watanzania wameyaona matokea yake .
Kuongezeka
kwa utalii wa ndani umefungua fursa kwa vijana wa kitazania na makapuni ya
utalii kufanya kazi misimu yote ya mwaka.
Judith
Ngowello anasema wamejifunza mambo mengi
na kupongeza ubunifu ulioanzishwa na kampuni ya Zara Tours kwa kuanzish kampeni
ya “twende zetu Serengeti”kampei inayowalte watanzania pamoja .
“Jambo la
kipekee na ambalo halitafutika kwenye
historia yetu ni watoto wetu kujionea
wanyama kwa macho tofauti na awali
ambako walikuwa wakiwaona kupitia luninga”
Zara tours
ndiyo kampuni pekee ambayo imejijengea
uzoefu kwa Zaidi ya miaka 30 ikiwa na
uzoefu wa kuhudumia wageni wa ndani nan je ya nchi wakiwamo watoto .
Moureen Robert ni mmoja wa watoto
waliotembelea hifadhi hizo na kujioa vivutio vya utalii.
Anasema wamejifunza mengi na mbali ya kuona wanyama wakubwa
kama,tembo,simba,twiga,pundamilia,nyati,faru,chui,ngiri,duma,swala,viboko na
ndege pia walifurahia utalii huo kupitia
kampeni hiyo ya “ twende zetu Serengeti”.
Anasema walizoea
kuwaona wanyama hao kupitia vipindi vya television lakini kupitia kampeni hiyo ya
twende zetu Serengeti wameshuhudia
maajabu na wamejifunza mengi.
Hifadhi ya
taifa ya Serengeti ni moja ya Hifadhi Tano(Big Five}ambazo zimekuwa zikiingiza
watalii wengi na kuliingizia taifa fedha za kigeni.
Katika mwaka
wa fedha wa 2023/2024 watalii 1.451,176 walitembelea hifadhi za Taifa ikiwa ni
takwimu zilizofikia mwenzi februari mwaka jana huku Serengeti ikiongoza kwa
idadi kubwa ya wageni.
Mwisho…..
0 Comments