Safina Sarwatt,Moshi,
CHAMA cha Mapinduzi (CCM ) wilaya ya Moshi M
jini Mkoani wa Kilimanjaro, kimeunga mkono maamuzi ya mkutano mkuu wa CCM Taifa uliofanyikika Tarehe 18-19/01/2025, kwa kuwapitisha wagombea wa Urais, Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea mwenza wa urais pamoja na Dkt.Hussen Ally Mwinyi kuwa Mgombea urais wa Zanzibar.
Mkutano huo ulifanyika kwenye soko la nafaka la Mbuyuni Mjini Moshi na
kuhudhuriwa na wanachama wa chama hicho,wafanyabiashara wa soko hilo pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali.
Akizungumza katika mkutano huo mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Seleman Mfinanga alisema kuwa katika uongozi wa rais Dkt Samia Suluhu Hasan mkoa huo umepokea fedha nyingi kwa ajili mirandi mbalimbali ya maendeleo.
Alisema kuwa ndani ya miaka minne ya uongozi wa Dkt.Samia Suluhu Hasan mkoa wa Kilimanjaro ulipokea fedha zaidi ya billion 956.63 kwa ajili ya miradi ya maendeleo 1,360.
“Sekta ya afya billion 117,Elimu billion 149.64,Ujenzi billion 125.46,Maji billion 370.87,Nishati billion 67.2,wateja waliounganishiwa umeme na Tanesco 98,9,wateja waliounganishwa huduma ya umeme kupitia Rea 5352,Utalii billion 4.62,Kilimo na Mifungo billion 28.36,”alisema Mfinanga.
Mfinanga aliwashukuru wananchi kwa kukipigia kura chama cha mapinduzi(CCM)katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka jana na kuwaomba kuendelea kukiamini na kumpa kura nyingi Rais Dkt Samia Suluhu katika uchaguzi mkuu ujao mwezi Oktomba ,
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu alisema serikali tayari imetoa fedha Zaidi ya billion 489 kwa ajili ya upanuzi wa barabara kuanzia eneo la Holili wilayani Rombo hadi Daraja laa kikavu wilaya ya Hai.
Alisema Moshi mjini itajengwa km 15 za barabara 4 pamoja na ujenzi wa daraja mpya la kikavu na kwamba daraja la zamani halitavunjwa nabadala yake litatumiwa na wananchi.
Babu aliwakata wananchi na wafanyabiashara katika soko la Mbuyuni kutumia soko hilo ambalo limejengwa miondombuni ya kisasa bila ubaguzi na kila mmoja kurudi katika nafasi yake kwa utaratibu wa awali.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Moshi Zuberi Kidumo alisema manispaa hiyo itaweka utaratibu wa wafanyabishara wa karoti kwa kuwapangia eneo lenye miundombinu rafiki kwa ajili ya kuosha karo zao kabla kupelekwa sokoni.
mwisho….
0 Comments