SERIKALI imepatia ufumbuzi wa tatizo la muda mrefu la wanafunzi kata ya Toloha wilayani Mwanga kutembea umbali mrefu kwenda kusoma shule ya sekondari ya kata ya kwako Kwangu sekondari, hali ambayo imekuwa ikihatarisha usalma wao kutokana na wanyama wakali tembo.
Kufuatia changamoto hilo serikali imejenga shule mpya ya kisasa ya kata ya Toloha ambayo itakwenda kumaliza tatizo na kuongeza viwango vya ufaulu wa mitihani wilayani humo.
Akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule hiyo Mbunge wa Jimbo la Mwanga Joseph Tadayo amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya rais dr.Samia Suluhu Hassan wamepokea fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali,ikiwemo Elimu,Afya,Maji,na barabara.
Tadayo amesema kuwa ujenzi mradi huo wa shule mpya ni miongoni mwa ahadi ya ilani ya uchaguzi mwaka 2020/2025,na kwamba wilaya hiyo imepewa shule mpya za kata mbili,ikiwemo Toloha na Kivisini.
Amesema kuwa kata hiyo inachangamoto wanyama wakali tembo hali inayoĥatarisha usalama wanafunzi na kwamba kujengwa kwa shule hiyo itakwenda kupunguza adha hiyo.
Amesema kuwa mwaka 2020 wakati akiomba kura alitoa hadi ya kujenga shule pamoja na kufungua lango la kuingia hifadhi ya wanyama ya Mkomazi na tayari lango limeshafunguliwa na hivyo kuwataka wananchi hao kutumia bursa hiyo kujipatia fedha za kigeni.
Awali akitoa taarifa ya miradi ya elimu afisa elimu sekondari wilaya mwanga Ashimun Mzava ,amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa rais Dr.Samiah Suluhu Hassan idara ya elimu sekondari imepokea fedha kiasi shilingi. 5,893,531,372 kwa ajili ya ujenzi ya matundu ya vyoo 161,nyumba moja ya walimu 2/1 ujenzi wa mabweni 16,shule mpya ya kata 2 ,maabara 15,vyumba vya madarasa 67 na mabwalo mbili.
Mzava amesema wilaya pia imepokea fedha kiasi cha shilingi 98,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 1 ya walimu 2/1 ujenzi wa bweni 1 shilingi 130,000,000 na ujenzi shule mpya shilingi 584,280,028.
Amesema miradi hiyo bado haijaanza kwani fedha hizi bado zimepokelewa mwisho mwa mwaka wa fedha uliopita na mifumo bado hajafunguliwa.
Amesema uboreshaji wa miuondombinu na ongezeko la walimu limeendelea sambamba na uboreshajiwa taalumu na kngezeko la ufaulu katika shule.
Aidha amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ya rais Dr.Samia Suluhu ufaulu wa wanafunzi katika mitihani wa kidato cha nne umeongezeka kutoka 95% mwaka 2021 97%mwaka 2023 na ubora wa ufaulu kutoka 50.6%mwaka 2021 hadi 55%mwaka 2023.
"Kidato cha sita 2021 hadi 2023 ufaulu ulikuwa ni 100% kila mwaka,"amesema .
Amesema shule ya sekondari Toloha ni miongoni mwa shule za kata zilizopokea fedha za ujenzi ambapo shilingi 584,280,028 zilipokelewa kwa ajili ya ujenzi vyumba vya madarasa 8,jengo la utawala,jengo la tehama,maktaba,maabara za masomo ya sayansi,(Chemistry, biology na physics, pamoja na matundu ya vyoo 4 wanafunzi wa kiume 4 na wa kike.
Amesema shule tayari imeshasajili wanafunzi wa kidato cha kwanza na wameanza kusoma baada ya miuondombinu ya muhimu ya awali kukamilika.
Amesema tumefanikiwa kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za mwalimu 2/1 na ujenzi wake utaanza mara moja baada mufumo ya fedha kufunguliwa.
Amesema kujengwa kwa shule hiyo itakwenda kupunguza adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda shule sekondari ya kata ya kwako Kwangu sekondari ambayo ni mbali huku usalama wanafunzi ukiwa ni mdogo kutokana na wanyama wakali .
Amesema kutokana na uwepo wa wanyama wakali shule inahitaji mabweni mawili ya wasichana na wavulana sambamba na uzio kwa ajili ya usalama wanafunzi hivyo tunaomba utusaidie kuiombea fedha .
Amesema shule ya Toloha imesajiliwa rasmi Juni 21,2024 na kupata usajili S.6636 hivyo kuruhusu kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza Julai 1, 2024.
Mwisho......
0 Comments