SERIKALI YA KAMILISHA MADARASA YA KIDATO CHA TANO ,SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA YA DR.ASHAROSE MIGIRO




 


Mbunge wa jimbo la Mwanga (CCM)Joseph Tadayo ameweka jiwe la msingi ujenzi wa vyumba vya madarasa ya kidato cha tano ya shule ya sekondari ya Dr.Asharose Mingiro .





Akizugumza mara baada ya kukagua majengo hayo na kuweka jiwe la msingi mhe. Tadayo ameeleza kufurahishwa na ujenzi wa majengo hayo ya kidato cha tano pamoja na choo matundu 10na mabweni mawili na ofisi tatu.








Mradi  huo wa ujenzi wa vyumba sita vya madarasa, Mabweni mawili ,ofisi tatu na vyoo matundu 10 ilifanikiwa kupata fedha kutoka serikali kuu shilingi 429,000,000/=.

Aidha Januari 2024 serikali ilitoa fedha kwa ajili ya mradi huo ambapo ujenzi wake ulianza January 17,2024 na mradi upo katika hatua ya umaliziaji.






Awali akisoma taarifa ya mradi ujenzi wa vyumba vya madarasa kidato cha tano na mabweni pamoja vyoo mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana ya Dr.Asharose Mingiro,mwl.Flaviana Safari amesema Januari 2024 serikali ilitoa fedha kwa ajili ya mradi huo ambapo ujenzi wake ulianza January 17,2024 na mradi upo katika hatua ya umaliziaji.







"Ujenzi wa madarasa sita na ofisi tatu ya kidato cha tano fedha zilizotegwa 150,000,000/=fedha zilizotumika148,492,0798.86,kazi inayoendelea utegenezaji wa meza na viti vya wanafunzi,  mradi upo katika hatua ukamilishaji,"amesema. 





"Ujenzi wa mabweni mawili ya kidato cha tano,shilingi 260,000,000.,fedha zilizotumika 250,108,194.60 =/kazi inayoendelea kuweka sakafu,kuweka tiles chooni na bafuni,kuchorea jengo nje,kupaka ranging awamu ya pili,kuchimba na kujengea mashimo ya maji takana kuweka vifaa vya umeme awamu ya pili kuweka titania na magodoro,"amesema.












"Ujenzi wa choo matundu kumi ya kidato cha tano,fedha 19,000,000,fedha zilizotumika mpaka sasa ni shili18,786,013.50, ujenzi umekamilika,"amesema.








Shule ya sekondari ya wasichana nimiongoni mwa shule bora inayofanya vizuri katika mitihani za taifa kila mwaka.





Amesema mradi huu unaiwezesha shule kutoa mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia ambapo unawezesha watoto wa kike wa kitanzania  kutimiza ndoto zao.

Mwisho...

Post a Comment

0 Comments