Safina Sarwatt,Kilimanjaro.
MSIMU wa 23
wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon 2025
umezinduliwa mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Salinero-Kilimanjaro, iliyoko
Moshi, mkoani Kilimanjaro katika hafla iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa
michezo, kabla ya tukio hilo maarufu la kimataifa ambalo linatarajiwa kufanyika
Februari 23, 2025.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, aliyewakilishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Kiseo Yusuf Nzowa, alitoa pongezi kwa wadhamini, wandaaji na wadau wengine wa michezo kwa kufanya mashindano hayo kuwa endelevu, jambo ambalo limechangia kiasi kikubwa kuuweka Mkoa wa Kilimanjaro katika ramani ya dunia.
RC.Babu
amesema kuwa mbali na kukuza afya ya watu na kukuza michezo, mbio hizo ambazo
sasa ni maarufu Barani Afrika pia zinachangia kukuza uchumi wa Mkoa wa
Kilimanjaro na Taifa kwa ujumla kupitia sekta ya utalii kila mwaka, kutokana na
washiriki wa ngazi zote wanaokuweko mkoani Kilimanjaro kipindi chote cha mbio
hizo.
“Tunajivunia
mbio za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon ambazo zimeendelea
kuwa maarufu kila mwaka; tukio hili kwa sasa limekuwa maarufu huku
likiwashirikisha zaidi ya watu 12,000 na idadi kama hiyo ya mashabiki wanaokuja
mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kulifuatilia”, alisema na kuongeza, tukio hili
linawaleta pamoja watu kutoka takribani nchi 56 jambo ambalo linayafanya
mashindano hayo kuwa ya kipekee ukanda wa Afrika Mashariki na ya Kati.
Mkuu wa Mkoa
Babu alitoa rai kwa wadau wote wa michezo kushirikiana kwa Karibu na waandaaji
wa mbio hizo ili ziendelee kuleta manufaa zaidi ya kiuchumi kwa Mkoa, Taifa na
kwa mtu mmoja mmoja kutokana na ukweli kwamba mashindano hayo yanazidi kukua na
sambamba na umaarufu wake kuendelea kukua kila mwaka.
"Mbio
hizi huandaliwa kila mwaka na mwaka huu ni msimu wake wa 23, manafuaa yake
kiuchumi yanaonekana wazi kwa jamii yote ya Watanzania, kutokana pamoja na
mambo mengine kukua kwa biashara mbalimbali hususan katika mji wa Moshi; nitoe
wito kwa wafanyabiashara wote wa Moshi na Mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla
kuhakikisha wanazingatia ubora katika kutoa huduma zao ili kulinda heshima ya
Mkoa katika nyanja za kibiashara”, alisema.
“Nichukue
fursa hii kuwapongeza wadhamini wote wa mbio hizi wakiongozwa na mdhamini mkuu
Kilimanjaro Premium Lager ambao wanadhamini mbio za kilomita, kampuni ya YAS
ambao wanadhamini mbio za kilomita 21 (Yas Half Marathon) pamoja na Benki ya
CRDB ambao wanadhamini mbio za kilomita 5”, alisema.
Aliongeza,
“Napenda pia kuwaponegza wadhamini wengine ambao wanaunga mkono mbio hizo ambao
ni pamoja na kampuni ya saruji ya Simba (Simba Cement), Kilimanjaro Water,
TotalEnergies, kampuni ya TPC Sugar Ltd, Wasambazaji rasmi GardaWorld, CMC
Automobiles, Salinero- Kilimanjaro, Kibo Palace Hotel na Keys Hotel, ambao
ushiriki wao umechangia kuendelea kukua kwa mbio hizi”.
Akiongea
katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
Khensani Mkhombo, alisema kuwa kampuni hiyo inajivunia kuwa wadhamini wa mbio
hizo kwa miaka 23 iliyopita kupitia Bia ya Kilimanjaro Premium Lager na
kuifanya kampuni hiyo kuwa mmoja wa wadhamini wa muda mrefu kwenye tukio moja
la kimichezo hapa nchini.
Mkurugenzi
huyo aliendelea kusisitiza ya kuwa udhamini huo pamoja na kuboresha ya watu
pamoja na sekta ya michezo, pia umelenga kukuza uchumi wa Taifa kupitia sekta
ya utalii kwa kuitangaza Tanzania na vivutio vyake kila msimu wa mbio hizi
unapowadia.
“Kutokana na
mbio hizi kuzidi kupata umaarufu, Mwaka huu, kamati ya maandalizi ya mbio hizi
imekuja na mkakati mpya unaolenga kufanya matamasha ya utangulizi ambayo yatakayofanyika
siku za mwisho wa wiki kuelekea mbio hizi, amapo matamasha hayo yataanza Ijumaa
na kumalizika Jumapili ambayo ndiyo siku ya mbio hizo”, alisema na kuongeza,
matamasha haya yanatarajiwa kuboresha biashara mjini Moshi.
Akizungumzia
kuhusu zawadi zilizoandaliwa kwa msimu wa 2025, Mkhombo alisema kuwa
Kilimanjaro Premium Lager imetenga jumla ya shilingi milioni 30, ambapo
washidni wa kilomita 42 kwa wanaume na wanawake kila mmoja anatarajiwa kupata
zawadi ay shilingi milioni 5.5, ambapo wanariadha wa Kitanzania ambao watashika
nafasi ya kwanza katika mbio za kilomita 42watapata bakshishi ya 550,000/- kila
mmoja.
Akizungumzia
mafaniko mengine, Mkhombo alisema mbali na kukuza sekta ya michezo, mashindano
hayo pia yameimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya wadhamini, wandaaji,
chama cha riadha nchini RT pamoja na jamii yote kwa ujumla.
Kwa upande
wake, Afisa Mkuu wa Biashara YAS, Isack Nchunda alisema, "Mwaka huu
tunaadhimisha na kujivunia kuwa sehemu ya udhamini wa mbio hizi maarufu Barani
Afrika kwa muongo wa kumi sasa, kupitia udhamini wetu wa mbio za kilomita 21
maarufu kama Yas Half Marathon, ambapo kitengo hiki kinawaleta washiriki
takribani 6,500, wakiwemo wanariadha maarufu Barani Afrika”.
Alisema
mwaka huu, wakimbiaji na washiriki wengine wa pembeni kwa maana ya mashabiki wa
mbio hizo watarajie kuona mambo mazuri kwenye mbio za kilomita 21 kutokana na
uzoefu walionao wadhamini wambio hizo ambao ni Yas, ambapo alitoa rai kwa
washiriki wa mbio hizo kujitokeza mapeam kuwahi nafasi zao kabla mbio hizo
hazijaanza siku ya tukio hilo.
Kwa upande
wao kamati ya waandaaji wa mbio hizo waliwashukuru wadhamini wakuu wa
Kilimanjaro Premium Lager na YAS kwa kutenga kitita cha jumla ya shilingi
milioni 53 ambazo zitatolewa kama zawadi ya Mbio za kilomita 42 na kilomita 21,
pamoja na vitengo vinmgine mbalimbali.
Waandaaji
hao pia walisema kuwa tukio hilo mwaka huu, pia linalenga kuchangia asilimia 5
ya kila malipo ya kiingilio kwa ajili ya msaada kwa Shirika la Tumaini la
Maisha (TLM), msaada ambao wamesema unalenga kuwahudumia watoto wanaougua
ugonjwa wa saratani ili wapate matumaini mapya baada ya kupata matibabu ya
ugonjwa huo.
“Pesa zote
ambazo zitachangwa kwa ajili ya msaada huo mwaka huu, zitaelekezwa kwenye Kituo
cha Matibabu ya saratani wka watoto kilihcoko katika hospitali ya rufaa ya
kanda ya KCMC (KCMC ZRH) iliyoko Moshi, mkoani Kilimanjaro”, ilsema sehemu ya
taarifa ya wandaaji hao.
Mbio za
Kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zinatarajiwa kufanyika Jumapili
ya Februari 23, 2025, katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU),
ambapo mbio hizo zimeadnaliwa na kampuni ya Kilimanjaro Marathon na kuratibiwa
hapa nchini na kampuni ya Executive Solutions Limited, ambapo kampuni ya Wild
Frontiers ndiyo inawajibika na matayarisho yote ya usafiri pamoja na maswala
yote ya masoko yanayohusiana na tukio hilo muhimu.
MWISHO
0 Comments