CCM Moshi Mjini Yaendelea na Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

moshi


Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Moshi Mjini kimeendelea na kampeni zake za uchaguzi wa serikali za mitaa, unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024. Katika kampeni za kata ya Karanga, CCM imekinadi ilani yake ya utekelezaji, ikionesha mafanikio mbalimbali yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kata ya Karanga ni miongoni mwa Kata  21 ya kata za Manispaa ya Moshi mkaoni Kilimanjaro,ambapo kata hiyo ina mitaa miwili,Katanini na mtaa wa Magereza.

Wagombea katika yote miwili wameoneka kukubalika kwa mujibu wa wananchi kutokana na kwamba wote wanatetea nafasi zao.

Mtaa wa Katanini,Esther Nkiisa, anayegombea kipindi cha pili mfululizo, na alipita bila kupingwa katika kura za ndani ya chama.

Mtaa wa Magereza,Ramadhan Nyamsera, ambaye amedumu kwa vipindi vinne, alipata ushindi mkubwa katika kura za chama kwa kura 97 dhidi ya wagombea wawili waliopata kura 3 na 2 mtawalia.



Diwani wa kata ya Karanga, Deogratius Mally  ameonyesha imani kubwa kwamba CCM itashinda kwa asilimia 99 kutokana na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo, ikiwa ni pamoja 

amesema kuwa katika kata hiyo serikali imetekeleza ilani ya CCM kwa asilimia kubwa na kwamba wananchi wameendelea kuwa na imani na chama tawala na  kuahidi kuendelea kukipigia kura cha hicho.

Alisema katika miradi  ya Miundombinu barabara kata hiyo serikali ijenga barabara tatu kwa viwango vya lami barabara moja kwa kiwango cha Changarawe huku barabara mpya 12 zimefunguliwa .


Amezitaja Barabara hizo kuwa  Barabara ya Magereza–Shimatunda (mita 800),Barabara ya Karanga Mishen One (mita 800),Barabara ya Ndesiangawa (Boisafi Road, mita 700).


"Barabara  ya Victoria (kilomita 1.7) kiwango cha changarawe,baarabara ya amani center ,na barabara mpya 12 zimefunguliwa na zimeweka katika mipango wa kujengwa kwa viwango vya lami,hivyo basi sisi kama wadau na viongozi wa wananchi tuna kila sababu ya kusema Rais Dr.Samia mitano tena bila kuwoga wowote,"alisema Deogratius .

 


Miradi ya Elimu.


Ukarabati wa madarasa mawili katika Shule ya Msingi Magereza..Ujenzi wa matundu ya vyoo,Matundu 16 (wavulana 8 na wasichana 8).



Uwezeshaji wa Jamii:

Kurudishwa kwa mpango wa TASAF katika mtaa wa Katanini, ambao ulikuwa umeondolewa kwa muda mrefu.


Ushindi wa CCM Watarajiwa

Diwani Deo Mally alisisitiza kwamba mafanikio haya yanatoa matumaini makubwa ya ushindi kwa wagombea wa CCM. Aidha, alieleza kuwa miradi hii ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za ilani ya uchaguzi wa mwaka 2020, inayolenga kuboresha maisha ya wananchi kwa ujumla.

Uchaguzi huu unatarajiwa kuwa kipimo cha umaarufu wa CCM na mwendelezo wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika ngazi ya mitaa.

Post a Comment

0 Comments