Dodoma,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amefungua kikao cha 39 ya Jumuiya yaTawala za Mitaa Tanzania(ALAT),uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention center jijini Dodoma.
Akizungumza wakati akufungua mkutano Rais Dkt.Samia aliwataka wajumbe hao kwenda kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja suala la ukusanyaji wa mapato ya serikali katika halmashauri zao.
"Hakikusheni mnasimamia vema ukusanyaji wa mapato katika maeneo yetu mkifanya hivyo mapato ya serikali yataongezeka na miradi ya maendeleo yatatekelezwa kupitia mapato hayo,"alisema Rais Dkt.Samia.
Amesema kuwa kuna baadhi ya maeneo Kuna mifumo ya pembeni ya wakusanya mapato lakini hayafiki serikalini kusababisha fedha kupotea.
"Hakikusheni mnadhibithi mianya hiyo ya upotevu wa fedha zinakunywa za mapato,"alisema
Rais Dkt.Samia alisema serikali ya awamu ya sita imeweza kutekeleza miradi mikubwa kwa asilimia kubwa na kwamba hayo nikutokana na usimamizi mzuri wa miradi hiyo.
Katika hatua nyingine Rais Dkt aliwapongeza wajumbe mkutano mkuu wa 39 ALAT kwasimamizi mzuri miradi ya maendeleo.
Nae Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa amesema Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ni muhimili wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.
Mchengerwa alisema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonesha dhamira ya dhati ya kuhakikisha ALAT inaimarika kwa kupeleka fedha nyingi, vifaa, watumishi na mahitaji mengine kwenye halmashauri ili wananchi waweze kupata hudums kwa urahisi.
"Mheshimiwa Rais tunapokusanyika hapa chini ya mwamvuli wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa yaani ALAT, tunafanya hivi tukiwa na shauku na matumaini makubwa ya kuona ALAT ni muhimili muhimu wa utekelezaji wa maono yako kwa Taifa letu la Tanzania.
" Mheshimiwa Rais, kama alivyosema Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, maendeleo ni kazi, si bahati. Taifa lisilo na nidhamu ya kazi haliwezi kujikwamua. Ndoto za maendeleo hazijengwi kwa maneno tu bali kwa vitendo na dhamira thabiti. Historia ya nchi yetu zimejaa ndoto kubwa zilizoasisiwa na waasisi wetu, na leo hii tunashuhudia ndoto hizo zikigeuka kuwa halisia. Tumepiga hatua kubwa na kufanya yale ambayo yalidhaniwa hayawezekani, lakini chini ya uongozi wako (Rais Dkt. Samia), yamewezekana" alisema Mchengerwa.
Mchengerwa alisema maendeleo sio ahadi bali ni hatua anazochukua mtu kila siku, na hilo linahusisha utekelezaji wa vitendo katika mchakato wa maendeleo, hivyo viongozi wa Serikali wanapaswa kujua kila ahadi inayotolewa inatakiwa ifanyiwe kazi ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
Mwenyekiti wa ALAT Taifa Murshid Ngeze amesema katika kipindi cha Rais Dkt. Samia, Serikali za Mitaa na chombo cha ALAT vimeimarika sana kwa sababu ameweza kuviwezesha kuanzia huduma za jamii na shughuli za maendeleo kwa kupeleka fedha nyingi za miradi.
Ngeze alisema hata kimapato, halmashauri zimekuwa zikiongeza mapato mwaka hadi mwaka, kwani mwaka wa fedha 2023/24 hadi mwezi Machi halmashauri ziliweza kukusanya sh. bilioni 848.3, na makisio ya mwaka wa fedha 2024/25 wamekusudia kukusanya sh. trilioni 1.3 jambo ambalo linaonesha mapato ya halmashauri yanaongezeka.
Ngeze alitoa ombi kwa Rais Dkt. Samia ya kuzipatia magari Idara ya Maendeleo ya Jamii, Kitengo cha Sheria na Ukaguzi wa Ndani, kwani wakipata magari hasa Idara ya Maendeleo ya jamii, itasaidia kufuatilia fedha zile za halmashauri za asilimia 10 ambazo zinakopeshwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Ngeze alisema hadi Machi, 2024 sh. bilioni 222 zilikuwa nje kwa wakopaji, hivyo kama Idara itakuwa na gari itaweza kufuatilia ili zirudishwe na watu wengine waweze kukopa.
MWISHO.
0 Comments