Safina Sarwatt, Same.
MWAKA 2013 kanisa katoliki jimbo la Same lilianzisha shule ya sekondari ya wavulana ya mchepuo wa Sayansi ya Mtakatifu Joachim ikiwa ni mkakati wa kanisa hilo kupanua wigo wa wataalamu wa masomo ya sayansi.
Malengo ya kuanzishwa kwa shule hiyo ni pamoja na kuwawezesha vijana wa kitanzania kupata huduma bora ya elimu pamoja na malezi bora ikiwa ni mkakati wa kuleta mageuzi makubwa kwenye maendeleo ya Taifa.
Lengo jingine ni pamoja na kukabiliana na changamoto ya upungufu wa watalamu wa masomo ya sayansi wakati Taifa likielekea katika uchumi wa viwanda ikiwa ni moja ya malengo mahususi ya Taifa.
Katika mahojiano maalumu na mwandishi wa Makala haya,Askofu mkuu wa Jimbo katoliki la Same mhashamu Baba Askofu Rogate Kimaro ameelezea namna walivyoweza kufanikisha maono ya kuanzishwa kwa shule h iyo.
ambaye ndiye mlezi wa shule shule hiyo ameeleza namna ambayo wameweza kufanikisha maono hayo.
Askofu Kimaro ambaye pia ndiye mlezi wa shule hiyo,alikuwa akizungumza na mwandishi wa makala haya wakati wa shukrani ya kusherekea miaka 10 ya kuanzishwa kwa shule hiyo hivi karibuni.
Anasema wakati wa kuanzishwa kwa shule hiyo walipia changamoto kadhaa lakini walifanikiwa kuzishinda kutokana na kumtanguliza mwenyezi mungu pamoja na nia ya dhati katika kutoa huduma kwa lengo la kuisaidia jamii.
Anasema mwaka 2013 serikali ilitoa kibali kwa kanisa hilo lililowezesha usajili wa shule kuendelea na kuishukuru serikali kwa kuendelea kuziamini taasisi za dini.
Anasema mbali na misaada ya wadau na wazazi shukrani kubwa wanazielekeza kwa serikali ya Italia kutokana na msaada mkubwa wa kifedha pamoja na kuwapa faraja kubwa katika kuyafikia malengo.
"Licha misaada ya wazazi na wadau fedha zingine tumepata kutoka serikali ya Italia,serikali za nchi za wenzetu huwa wanasaidia sekta binafsi,kweli ilikuwa jambo la faraja sana kuona serikali inasaidia sekta binafsi,"anasema Askofu Kimaro.
Askofu Kimaro amesema Taifa ambalo Lina dira ya maendeleo ni lazima ili na maono ya kuboresha huduma ya elimu ili iweze kuendena na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Anasema kanisa katoliki Jimbo la same limeona ni vema kujikita zaidi kutoa elimu bora na malezi kwa vijana wa kiume ili kuweza kuleta mabadiliko mabadiliko na ufanisi mkubwa kwenye Taifa.
Amesema Taifa linahitaji watalaamu wengi wenye uwezo na ufanisi mkubwa ili waweze kuendana na soko la ajira la dunia kwani ni tupo katika kipindi ambacho Taifa linahitaji kupiga hatua zaidi kimaendeleo.
"Taifa ambalo halina maono ni Taifa ni mfu linahitaji kuamka usingizini pia vijana waliwa bora watakuwa wazazi bora wa baadae wataweza kuleta familia pamoja wazazi,"amesema.
"Vijana wengi wanazurura hawapendi kazi lakini pia kuna wazazi hawapendi watoto wao wafanye kazi kwamba hii siyo njia bora tunawafundisha kazi ili wawe Taifa bora ya baadae,"amesema.
"Tunapo kataa wasifanye kazi tunategeneza kizazi za ovyo cha vijana wasiojiweza na wasio weza kuzalisha chochote na kwamba Taifa lolote duniani lisilokua na vijana wawajibikaji hilo taifa lina kwenda kuyumba kiuchumi,"anasema.
Akizugumzia suala la utunzaji wa Mazingira amesema wameotesha miti zaidi ya 4000,ambapo kila mwanafunzi anaotesha miti zaidi ya 15 na kumwangilia,"amesema.
Meneja mkuu wa shule hiyo Padre Deogratius Mchagi amesema Shule hiyo inafanya vizuri kwasababu tunajiamini natunachokifanya.
Amesema Wanafunzi wengi wamejengewa uwezo kubwa sana wakujiamini na namna ya kujibu maswali na kujieleza pia kujitegemea.
"Mafaniko yote hayo yametokana na jitihada zinazofanywa na uongozi wa shule kuwa makini na kazi na kuwapenda wanafunzi wote bila kuwa bagua kwa nataka,"amesema Padre Mchangi.
Amesema shule hiyo inamazigira bora ya kufundishia ikiwemo maabara za kisasa kwa masomo ya sayansi pamoja na vifaa vya maabara pia shule ina library yenye vitabu vya aina mbalimbali kwa ajili ya Wanafunzi kujitosomea.
Anasema mazingira ya shule ni tulivu kwa wanafunzi kujisomea ,pia walimu bora wenye ufanisi katika ufundishaji wa masomo ya sayansi.
Anasema wakati nchi yetu kwasasa inauhitaji kubwa ya watalamu kutokana na mabadiliko makubwa ya teknolojia na sayansi ili kuweza kuendana na soko la ajira ya ndani na nje ya nchi.
Anasema uzalishaji wa watalamu unaedana na sambamba na maadali ili kuleta ufanisi mkubwa wa kazi na Taifa kuendelea kupiga hatua kimaendeleo.
Anasema katika kulea watoto wa kiume wamegudua mambo mengi ikiwemo vipawa vya watoto.
Anasema shule hiyo iwekeza kuwajengea uwezo si tu elimu ya darasani na kwamba baada ya masomo ya darasani wanafundishwa kutegeneza mabwawa ya samaki na kufunga.
Shughuli nyingine waliofundishwa ni pamoja utunzaji wa mazingira kuandaa bustani za mboga mboga na matunda,kwani ndiyo njia pekee yakumwandaa kijana bora na viongozi wa kesho.
Wazazi kuwa katibu na watoto wasiamini katika kuwapeleka watoto shule inatosha nakuweza kutatua tatizo la watoto.
Lengo la shule ya mtakatifu Joachim nikuzalisha watoto wa vipaji ya kufanya kitu fulani.
Masomo ya vitendo si tu anafaulu tu darasani nikuendelea kile ambacho mtoto anacho lazima wafunishwe katika mazingira ya kuwajengea uwezo kuzalisha.
"Hao vijana tunaozalisha si tu wakwenda kukaa maofisini bali ni kwenda kutatua matatizo fulani,ndiyo maana ukiangalia katika shule yetu kila somo la sayansi ina mwalimu wake, kila mwalimu anadarasa la kwakwe,pia wanafunzi wajegewa uwezo wa kujiamini na,kuonyesha kile ambacho anaweza kufanya,"amesema .
Mkuu wa shule Charles shogolo tangu kuanzishwa mwaka 2013
Tumewekeza zaidi katika kuwajenga watoto wa kiume wa kitanzania ili kuongeza watalamu bora katika sekta ya sayansi ambayo bado kuna uhitaji mkubwa wa watalamu.
Mwl.Charles amesema kila mmoja anayefanya kazi katika taasisi hiyo amekuwa akifanya kazi kwa ufanisi na uweledi mkubwa,na kusimamia maadili ya kazi.
"Malezi bora na elimu bora
Mwanafunzi yoyote anayefundishwa na walimu wenye maadali lazima afaulu vizuri,"amesema.
Amesema kuwa shule hiyo imekuwa na viwangi vya juu katika ufaulu wa mitihani ya kidaifa kwa kidato cha pili na nne ambapo daraja la kwanza,pili na tatu na kwamba mpango ni kuwa kufuta daraja la tatu.
"Sisi shule yetu tulishafuta daraja nne na kwamba mpango ni kufuta kabisa daraja la tatu na kubaki na ufaulu wa daraja kwanza na pili ,"amesema.
Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Angella Kessy amesema Wazazi wanafurahia sana shule hii wengi watoto wao wamesoma hapa kuanzia mtoto wa kwanza hadi watatu.
Anasema wanafunzi wanaomaliza masomo katika shule hii wanamaadili mema.
Pia ametoa wito kwa wazazi hasa katika kipindi hiki wazazi wengi wanakuwa na majukumu mengi wanatoka asubuhi nakukosa muda wa kulea familia na wadada wa kazi majukumu yote,kuacha tabia hiyo hivyo tenga muda kidogo kwa ajili malezi ya watoto.
Anasema Wazazi wanapaswa kutafakari walipoteleza na kuanza upya majukumu yao.
0 Comments