Safina Sarwatt,Mohi,
Zaidi ya wanafunzi 1000 wanaoishi katika familia duni wanaomaliza masomo ya sekodari na kufaulu kwenda vyuo vya ufundi na vyuo vikuu wamenufaika na ufadhili wa kiwanda cha sukari TPC Moshi kupitia taasisi yake isiyo ya kiserikali ya Foundation for Community Transformation in Kilimanjaro(FTK) kwa kipindi cha miaka 12 ambapo kila mwaka Zaidi ya wanafunzi 250 hupata ufadhili.
Wanafunzi hao ni wale wanaotoka katika familia duni kutoka vijiji vinavyoizunguka kiwanda cha Sukari TPC Moshi,ambapo kiwanda hicho kila mwaka hutenga Zaidi million 400 kwa ajili kuwa fadhili masomo ya elimu ya juu.
Aidha kiwanda hicho hutenga Zaidi ya billion 1.5 kupitia taasisi yake FTK kuhudumia wananchi zaidi 95000 wananchi eneo la Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro na wilaya Simanjiro mkoani Manyara wanaizunguka .
Sehemu ya fedha hizo zinakwenda katika ufadhili wa wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita na kushindwa kuendelea na maosmo ya elimu ya juu kutokana na familia zao kutokuwa na uwezo wa kulipia ada .
Mpango huo ulioanza mwaka 2012 hadi sasa umewezesha zaidi ya wanafunzi 1,000 wanaoishi kuzunguka kiwanda hicho katika wilaya ya Moshi Vijijini kunufaika na mpango huo ambao unatajwa kuwa utapandisha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi hao.
Msimamizi wa Shirika hilo,Lazaro Urio, amesema hayo katika hafla ya kukabidhi Mabweni na Maktaba kwa shule ya Sekondari TPC, ambayo ni kitengo cha uwajibikaji kwa Jamii (CSR) cha Kiwanda cha Sukari TPC iliyofadhili ujenzi wa shule, mabweni na miradi ya maktaba.
“Kabla ya ujenzi wa shule hizo, wanafunzi wengi wao wakiwa ni watoto wadogo walilazimika kutembea umbali mrefu kufika shule zilizo nje ya eneo la TPC”, alibainisha na kuongeza, ndipo wazo la kuanzishwa kwa shule mbili za sekondari za TPC na Shule ya Sekondari ya Chewe katika eneo hilo ilianzishwa.
Urio amesema kuwa, baada ya kujengwa kwa shule hizo mbili, changamoto nyingine iliibuka ambapo amesema, safari hii wanafunzi wengi kutoka nje ya eneo la TPC walilazimika kutembea umbali wa kilomita 14 hadi 20 kwenda na kurudi kutoka katika shule hizo mbili.
"Ili kukabiliana na changamoto hiyo, FTK ilikuja na wazo lingine la kulipia usafiri wa wanafunzi kwa kukodisha mabasi, ambapo wazazi walialikwa kuchangia asilimia 50 ya gharama, lakini wengi hawakuweza kufanya hivyo kwa sababu mbalimbali", alisema.
Kwa mujibu kiongozi huyo, kufuatia changamoto hiyo mpya FTK ilikuja na wazo la ziada la kujenga bweni katika shule ya Sekondari ya TPC kuchukua wanafunzi 68 waliokuwa wakitembea umbali mrefu kwenda na kurudi shule ya sekondari ya TPC.
“FTK iliamua kuwekeza katika shule ya Sekondari ya TPC kwa kujenga bweni jipya lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 68 kwa gharama ya shilingi milioni 147, ambapo uongozi wa shule ulipewa jukumu la kuweka vitanda kwa ajili ya bweni hilo”, alisema Urio.
Kuhusu maktaba mpya ya shule hiyo, Urio amesema ujenzi wake umegharimu Sh milioni 126 na kwamba itajumuisha maabara ya kompyuta.
“Maktaba hii haina thamani hivyo nitoe rai kwa wadau mbalimbali kuungana na FTK kukusanya jumla ya Sh milioni 25 ili kumudu gharama za thamani zote zinazohitajika katika maktaba hiyo mpya”,
0 Comments