Wanafunzi 68 wa kike wanaosoma shule ya kutwa ya sekondari TPC wanufaika na kiwanda cha sukari TPC


MAKALA ELIMU


 Safina Sarwatt,Mohi,



JENGO LA BWENI LA WANAFUNZI WA KIKE SEKONDARI TPC



Wanafunzi 68 wa kike  wanaosoma shule ya kutwa ya sekondari ya TPC ,wamefaidika na juhudi za kiwanda cha sukari cha TPC Moshi baada ya Kiwanda hicho  kujengwa bweni .

Hatua hiyo imewaondolea adha ya   kutembea umbali mrefu wa kilometa 20 kwenda na kurudi shuleni.
 






Uamuzi huu unasaidia kuboresha elimu kwa wasichana, kwani unawapa nafasi ya kujikita zaidi katika masomo yao bila wasiwasi wa safari ndefu na hatari walizokuwa wakikabiliana nazo.


Hii pia ni hatua muhimu katika kupunguza vikwazo  ambavyo vimekuwa vikiwakabili wasichana wengi katika kusaka  elimu, kama vile muktadha wa kijinsia na changamoto za usafiri.

 

 Kujengwa  kwa bweni hilo  kutawawezesha wanafunzi hao wa kike kujisomea kwa bidii zaidi kwenye masomo na kuongeza uwiano wa ushiriki wa mtoto wa kike  katika elimu.


Akizungumza katika hafla ya kukabidhi bweni hilo ,mtendaji mkuu wa kiwanda hicho anayeshugulikia masuala ya utawala katika kiwanda hicho , Jaffari Ally anasema kiwanda hicho kimekuwa kikitenga fedha kila mwaka kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya shule zilizopo kuzunguka kiwanda hicho.




JAFFARI ALLY-mtenda mkuu kiwanda cha sukari TPC 


 Jaffari ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya Taasisi Tanzu ya Kiwanda hicho ya   Foundation for Community Transformation in Kilimanjaro(FTK) anasema mbali na kukarabati miundombinu ya shule hizi,pia wamekuwa wakijenga shule hiyo ikiwa ni sehemu ya Kiwanda hicho kururdisha faida kwa jamii inayowazunguka.
 

Ally alisema kuwa shule ya sekondari TPC walifanya upembuzi yakinifu na kubaini changamoto kubwa ya ukosefu wa bweni hali ambayo imekuwa ikichangia wanafunzi wa kike kutembea umbli mrefu na kwenda na kurudi  na kurejea nyumbani usiku na kutishia  maisha yao.

Alisema wanafunzi wengi wa kike walikuwa wanatoka maeneo katanini kwenda TPC kusaka elimu kujipatia elimu .

Amesema hali hiyo ilikuwa ikiwafanya kutoka  majumbani mwao  alfajiri na kufika shuleni saa tatu asubuhi huko wakikosa baadhi ya vipindi.

 





“Mazingira yalikuwa hatarishi sana kwa sababu kuna mashamba makubwa ya miwa  wanapotoka shuleni jioni inawalazimu kutembea umbali wa kilometa zaidi ya 20 kwenda na kurudi majumbani ,tuliona hali hiyo ni hatarisha kwa watoto wa kike hivyo tukaona ni vema sasa tuwajengee bweni la wasichana ili waweze kusoma katika mazingira salama na waweze kufikia malengo yao,”alisema Jaffery.
 
"Leo hii tunakabdhi  Mabweni na Maktaba kwa shule ya Sekondari TPC, ambayo ni kitengo cha uwajibikaji kwa Jamii (CSR) cha Kiwanda cha Sukari TPC iliyofadhili ujenzi wa shule, mabweni na miradi ya maktaba",alisema .


Alisema kabla ya ujenzi wa shule hizo, wanafunzi wengi wao wakiwa ni watoto wadogo walilazimika kutembea umbali mrefu kufika shule zilizo nje ya eneo la TPC, ndipo wazo la kuanzishwa kwa shule mbili za sekondari za TPC na Shule ya Sekondari ya Chewe katika eneo hilo ilianzishwa.

alisema  kuwa, baada ya kujengwa kwa shule hizo mbili, changamoto nyingine iliibuka ya wanafunzi wengi kutoka nje ya eneo la TPC kulazimika kutembea umbali wa kilomita 14 hadi 20 kwenda na kurudi kutoka katika shule hizo mbili.



"Ili kukabiliana na changamoto hiyo, FTK ilikuja na wazo lingine la kulipia usafiri wa wanafunzi kwa kukodisha mabasi, ambapo wazazi walialikwa kuchangia asilimia 50 ya gharama, lakini wengi hawakuweza kufanya hivyo kwa sababu mbalimbali", alisema .

Kwa mujibu wa Jaffari, kufuatia changamoto hiyo mpya FTK ilikuja na wazo la ziada la kujenga bweni katika shule ya Sekondari ya TPC lenye uwezo wa kuchukua  wanafunzi 68 wa kike.
 

“FTK iliamua kuwekeza katika shule ya Sekondari ya TPC kwa kujenga bweni jipya lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 68 kwa gharama ya shilingi milioni 147, ambapo uongozi wa shule ulipewa jukumu la kuweka vitanda kwa ajili ya bweni hilo”, amesema Urio.

Kuhusu maktaba mpya ya shule hiyo, alisema  ujenzi wake umegharimu Sh milioni 126 na kwamba itajumuisha maabara ya kompyuta,ambapo inauwezo kusoma wanafunzi Zaidi 48 kwa wakati moja.

“Maktaba hii haina thamani hivyo nitoe rai kwa wadau mbalimbali kuungana na FTK kukusanya jumla ya
Sh milioni 25 ili kumudu gharama za thamani zote zinazohitajika katika maktaba hiyo mpya”,




 
Baadhi ya wanafunzi  wa  shule hiyo , Gladines Kimaro alisema kuwa walikuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kuchelewa kufika   shule saa tatu asubuhi huku wakikosa baadhi ya  vipindi vya masomo.

Alisema changamoto hiyo ya kutembea umbali  mrefu  baadhi yao walishindwa kuendelea na masomo kutokana na vishawishi walivyokuwa wanakutana navyo njiani  ikiwamo kurubuniwa na  madereva  wa boda boda wanaoliokuwa wakiwasaidia kuwabeba kwenda shule ama kurudi nyumbani.



“Sisi watoto wa kike tunakutana na vishawishi vingi sana wakati mwimgine tunatembea sana tunachoka kwani tunatoka nyumbani alfajiri na kufika nyumbani usiku wa saa mbili unakuta mzazi hakuelewi kabisa ,inatulazimu kupanda lifti ya boda boda ili kuwahi umridhishe mzazi lakini huku unayopitia ni siri yako,”alisema.


“Tunakishukuru sana kiwanda cha TPC kwa kutujengea bweni hili la wasishana kwani litakwenda kubadilisha maisha yetu  na kufikia malengo yetu ,tunaahidi tutakwenda kufanya vizuri zaidi katika mtihani ya taifa,”alisema.

Mkuu wa shule ya sekondari TPC mwl.Salehe Shaban alisema  baadhi ya wanafunzi walikuwa wakifika shuleni kwa kuchelewa na baadhi  kujificha vichakani wakiogopa kuadhibiwa hivyo kusubiri mpaka muda wa kutoka ufika warudi majumbani hali ambayo ilikuwa ikiathiri viwango vyao vya  ufaulu hasa kwa wanafunzi wa kike.
 

Alisema kuwa kabla kujengwa kwa bweni hilo la wanafunzi wa kike , kiwango cha utoro kilikuwa kikubwa  .

Alisema  hivi karibuni aliwakuta  baadhi ya   wanafunzi wakiwa wamejificha maporini muda wa vipindi vya masomo vikiendelea,na  kuongeza kuwa uwepo wa  bweni hilo itachangia  mafanikio makubwa ya ufaulu kwa wanafunzi.




MWISHO.....

Post a Comment

0 Comments