MBUNGE ZUENA AKUTANA NA WANAWAKE WANAOGOMBEA UENYEKITI WA MITAA MANISPAA YA MOSHI NA KUWAFUNDA..

 MOSHI. 


MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA KILIMANJARO,MHE.ZUENA BUSHIRI




MBUNGE wa viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri amekutana na wakinamama wanaogombea nafasi ya Uenyekiti wa mtaa kupitia Chama cha Mapinduzi manispaa ya Moshi na kuwatia moyo kuelekea kampeni zitakazozinduliwa kesho pamoja na uchaguzi Novemba 27 mwaka huu. 



Zuena alikutana na Wagombea hao leo katika Ofisi za Chama wilaya ambapo alisema kuwa, Chama hicho kimejipanga kuhakikisha kinashinda katika mitaa yote stini ya manispaa ya Moshi. 



"Ninyi wakinamama mmetuinua kimasomaso tunajua mmepitia vikwazo vingi mpaka kushinda katika kura za maoni sasa ni jukumu letu sisi kama chama kuhakikisha wagombea wote wanaopeperusha bendera ya CCM mnashinda kwa kishindo" Alisema Mbunge Zuena. 


Aidha Mbunge huyo aliwataka wagombea hao kushirikiana na kushikamana kwa pamoja na pale wanapokutana na changamoto wasisite kuwashirikisha viongozi wa chama kata na wilaya ili ziweze kupatiwa utatuzi. 



MWKT.UWT MOSHI MJINI THERESIA KOMBA




Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) manispaa ya Moshi, Theresia Komba aliwataka wagombea hao kuwa makini katika kujilinda wao wenyewe kwani wapinzani wao kwa sasa wameshapoteza dira ya ushindi hivyo wanaweza kuwafanyia chochote. 


Theresia alisema kuwa, serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa katika manispaa ya Moshi hivyo yapo mambo ya kwenda kuwaeleza wananchi ni kwanini wawachague wagombea wanaotokana na CCM. 


"Wagombea mnatakiwa kutembea kifua mbele kwani mambo mengi na makubwa yamefanywa na CCM sioni sababu ya kushindwa kushinda mitaa yote stini chama chetu tuendelee kushirikiana ushindi kwetu ni muhimu sana" Alisema Theresia. 


Wanawake waliopitishwa na chama cha Mapinduzi kuwania Uwenyekiti wa mitaa ni mitaa kumi kati ya mitaa sitini ya manispaa ya Moshi.

KATIBU WA UWT MOSHI MJINI CATHERINE SARWATT





Mwisho.

Post a Comment

0 Comments